Shetta ataja sababu ya kutengana na diamond

Msanii wa muziki Bongo, Shetta amefunguka kwanini kipindi hiki haonekani karibu na Diamond kama ilivyokuwa mwanzo.

Shetta amesema kwa sasa kinachowatenganisha ni biashara tu na hakuna zaidi ya hapo.
“Sidhani kama kuna bifu lakini mimi nafikiri biashara sababu mwanzo tulikuwa tunaishi kama washikaji lakini ikimbukwe sote ni wanamuziki ili kutafuta inabidi kila mtu apambane,” amesema.
“Siri ya biashara kila mmoja anataka kufanikiwa, kila mmoja anataka kuwa namba moja na kuna series za mafanikio. Automatic wewe kama mwanamuziki na sifaidiki na wewe kwa njia moja au nyingine, siwezi kukupa njia zangu na wewe huwezi kunipa njia zako lakini haiwezi kuwa kama tatizo,” Shetta ameiambia Wasafi TV.
Utakumbuka wawili hawa walishafanya ngoma mbili pamoja ya kwanza ilikwenda kwa jina la Nidanganye na nyingine ni Kerewa zote zikiwa za Shetta.
Source: Bongo 5
MaoniMaoni Yako