SANCHI: Sina Mpango wa Kurudi Tanzania


MWANAMITINDO mwenye umbo matata Bongo, Jane Ramoy ‘Sanchi’ amesema kuwa kwa sasa Wabongo watamsubiri sana kwani hana mpango wa kurejea nchini hivi karibuni.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Sachi ambaye yuko nchini Nigeria kwa kipindi kirefu, alisema kuwa, ameamua kubadilisha hali ya hewa na hana mpango wa kurejea nchini.

“Sasa hivi Bongo wanisamehe tu kwani sina mpango wa kurudi hivi karibuni, nimeamua kubadilisha hali ya hewa kabisa na niwaa-mbie tu, si kwamba kuna mwa-naume kanileta huku, nimekuja kivyang-uvyangu,” alisema. 
MaoniMaoni Yako