Samatta atua MakkaStraika Mtanzania anayekipiga klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta ametimiza moja ya nguzo za Kihislamu baada ya kwenda kuhiji mjini Makka.


Mbwana amefanikisha zoezi hilo ambalo hufanywa na sehemu kubwa ya waumini wa Kiislamu ambapo mtu anapokwenda Makka kwa ajili ya Kuhiji na anapokamilisha hupewa jina la Alhaji kwa mwaume.


Samatta ambaye muda wowote atatua nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya msimu wa ligi ya Ubelgiji kumalizika.


Hata hivyo, ameandaa mchezo maalumu kwa ajili ya kusaidia vijana mashuleni ambao utachezwa kati ya timu yake na ya msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba.