Wednesday, May 2, 2018

Safari ya yanga kuelekea algeria kesho ina shaka , viongozi hawapokei simu

Tags
Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuanza safari yake kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, kumekuwa na sintofahamu juu ya safari hiyo.

Licha ya sintofahamu iliyojitokeza,salehjembe imefanya jitahada za hali na mali kutaka kujua namna Yanga walivyojiandaa kuanza safari hiyo lakini viongozi wamekuwa hawapokei simu.

Yanga itakuwa na kibarua dhidi ya wapinzani hao wa Algeria, USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Mei 6 2018 nchini humo.

Haijajulikana sababu za viongozi hao kutopokea simu kwa takribani muda wa siku nzima ili kujua namna maandalizi yamefikia hatua gani kwa ajili ya safari hiyo.

Hata hivyo uongozi licha ya kushindwa kupokea simu, leo umetangaza kuitisha kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika majira ya saa 6 mchana kwenye makao makuu ya klabu.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz