Sababu ya Ramadhani Kabwili kuwekwa benchi Ngorongoro heroes ikipokea kichapo

Jana Jumapili Mei 13, 2018 timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ilifungwa 2-1 na Mali katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Afrika (AFCON) kwa vijana wa U20.

Kabwili ni miongoni mwa magolikipa vijana wanaofanya vizuri kwa sasa, katika mchezo kati ya Ngorongoro Heroes vs Mali Kabwili alikaa kwenye benchi jambo ambalo halikutarajiwa na wadau wengi wa soka nchini.

Kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje maarufu kama mzee wa ‘Always Next Time’ amezitaja sababu za Kabwili kuanza benchi katika mchezo huo.

“Kwenye timu wachezaji unawaangalia mazoezini halafu ndio unapanga timu, sasa Abdultwalib alifanya vizuri sana mazoezini ingawa alifanya mistake moja ya kutoa pasi haraka lakini mazoezini amefanya vizuri sana.”

“Kabwili amefanya mazoezi na sisi mara moja, sio fair kwa mchezaji ambaye amefanya vizuri mazoezini karibu wiki mbili umtoe umpange mtu mwingine.”

“Kabwili anauzoefu katika michuano ya kimataifa lakini mara ya mwisho amecheza lini? Alidaka akiwa Ngorongoro, akiwa Yanga hajadaka, ukiangalia Abdultwalib amedaka katika mechi mbili za kimataifa Kabwili kadaka mechi mbili za Congo DR.”

“Narudia tena, Abdultwalib kafanya vizuri mazoezini ndio maana nimempa nafasi ya kucheza. Kafanya makosa, tutaangalia makosa aliyofanya halafu tutaangalia namna gani ya kumsaidia ndio mpira upo hivyo.”

Hivi karibuni kulitokea mawasiliano duni kati ya  uongozi wa Yanga, TFF na Ammy Ninje jambo ambalo lilisababisha kutoelewana na Kabwili kuonekana kaikimbia Ngorongoro Heroes.

Source: Shaffih Dauda

MaoniMaoni Yako