Ronaldo atangaza kuondoka Madrid kiroho safi


Kiev, Ukraine. Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameweka wazi kwamba sasa anaweza kuondoka Real Madrid msimu huu wa kiangazi baada ya kuipa timu yake taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kikosi cha Zinedine Zidane kiliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp, mechi iliyopigwa jana Jumamosi usiku katika Jiji la Kiev, Ukraine.
Mabao mawili ya Gareth Bale na Karim Benzema yameifanya Real Madrid kuandika historia ya kutwaa taji hilo kwa mara tatu mfululizo.
Ronaldo mwenye miaka 33, ametwaa taji hilo mara tano akiwa na Real Madrid. Hata hivyo tayari ameonyesha hana muda mrefu kuitumikia klabu hiyo.
Alisema kwamba kwa kipindi chote ambacho amekuwa Real Madrid amekuwa  na furaha na baada ya wiki chache ataweka wazi kwa mashabiki wake kuhusu atachezea timu gani msimu ujao.
Credit: Mwananchi
MaoniMaoni Yako