Powered by Blogger.

Slider

Breaking

KITAIFA

VideoBar

This content is not yet available over encrypted connections.

KIMATAIFA

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

SPOTI TV

» » Real Madrid wagoma kufanya Guard Of Honour kwa Barcelona Leo! Hizi ndizo sababu zao

Barcelona wamenyakua taji la La Liga mwaka huu 2018, huku wakiwa na michezo mkononi. Hivi sasa kilichopo katika mipango ya Barcelona ni kulinda heshima na kuhakikisha kwamba wanamaliza michezo yao yote wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Ligi hiyo ya Uhispania.


Wanaokutana nao safari hii ni Real Madrid,ambao kwa desturi ya soka wanapaswa kuwapa Barcelona gwaride la heshima “The guard of honour”  lakini Madrid wameapa kwa maisha yao kwamba katu haitakuja kutokea kitu kama hicho eti wawape Barcelona gwaride la heshima.
Sababu hasa ya msingi haijaeleweka wazi lakini kumbukumbu zinatupeleka mwaka jana December, ambapo Real Madrid walikuwa wameshinda taji la klabu bingwa Duniani baada ya kuwafunga Gremio  goli 1-0 katika mchezo uliochezwa Abu Dhabi ambapo Ronaldo alifunga goli hilo la ushindi kwa timu yake ya Madrid.

Hilo lilikuwa ni kombe la tano katika mwaka wa 2017 baada ya kuwa tayari wameshinda Champions League, La Liga, Uefa Super Cup na Spanish Super Cup.
Baada ya ushindi huo kule Abu Dhabi, Madrid walipaa anga kurudi Uhispania ambako walipokelewa Kifalme na mashabiki wao na wahispaniola kwa ujumla kasoro Barcelona tu! Baada ya kurudi walikuwa na mchezo dhidi ya Barcelona wiki moja baadae.

Lakini katika mchezo huo ambao ndiyo ulikuwa wa kwanza toka warudi kutoka Abu dhabi walikorudi wakiwa na heshima ya Dunia, Barcelona wao waligoma kabisa kutambua heshima waliyonayo Madrid kana kwamba hawajui kilichotokea , hivyo walikataa katakata kuwapa Madrid Gwaride la heshima katika mchezo wao huo.

Kuna habari zinasambaa hapa Uhispania na Duniani kote kwamba Madrid wameamua kwa umoja wao kwamba hawatawapa Barcelona Gwaride hilo ikiwa ndiyo mchezo wa kwanza wa Barcelona toka walivyotwaa taji hilo la La Liga.

 Mchezo wa Barcelona na Madrid unatarajiwa kufanyika Leo hii mnamo saa Tatu na dakika arobaini na tano kwa masaa ya huko nyumbani Afrika Mashariki. 21:45. Muda huo ndiyo El Clasico inatarajiwa kuisimamisha Dunia pale wanaume hawa watakapokuwa wanaziumiza nyasi katika uwanja wa Camp Nou. Mchezo ambao Madrid wanataka kuharibu historia inayotaka kuwekwa na Barca, ya kumaliza Ligi yao bila Kufungwa hata mchezo mmoja.

SPOTI TZ, Lilimhoji Kocha wa Barcelona Valverde, kwamba anadhani kutokupewa gwaride la heshima ni kuikosea heshima Barcelona, alisema; “ mimi sifikirii hivyo”.


“Tumeshanyakua taji tayari, ndahani hilo ndilo la muhimu, kama tutapewa gwaride au la si jambo la maana sana kulizungumzia mara kwa mara” aliongeza kocha huyo ambaye amejitahidi sana kutokuongelea mchezo huo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post