Rayon Sports waichukulia Yanga kama timu dhaifu


Baada ya kuwasili nchini jana wakiwa na wachezaji wao wote muhimu kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Rayon Sports waeleza kuwa Yanga ni timu dhaifu.

Rayon wameeleza kuichukulia Yanga kama timu dhaifu kufuatia kushindwa kushinda jumla ya mechi zake saba zilizopita kwenye ligi na nje ya ligi.

Rayon wamesema kuwa wanaichukulia Yanga kwa namna hivyo huku wakiamini itakuwa mechi nyepesi kwao kupata matokeo.

Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho ukiwa ni wa pili kwenye hatua hiyo ya makundi.

Timu hiyo kutoka Rwanda ilienda sare ya bao 1-1 na Gor Mahia FC katika mchezo wa kwanza uliopigwa Kigali kwenye Uwanja wa Amahoro.

Wakati huo Yanga ilianza vibaya kwa kupoteza dhidi ya USM Alger jumla ya mabao 4-0 huko Algier, Algeria.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako