Ramadhani Malima Naye Asimamishwa Kuchezea Mbeya City

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, imetangaza kumsimamisha beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima, kwa kosa la kurudi Uwanjani kushangilia wakati akiwa amepewa kadi nyekundu.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 22 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Bodi imetangaza kumsimamisha mchezaji huyo kuichezea Mbeya City mpaka pale shauri lake litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF kisha kutolewa maamuzi.

Mchezaji huyo alipewa kadi ya pili ya njano na nyekundu kufuatia kucheza madhambi dhidi ya mchezaji wa Yanga zikiwa zimesalia dakika chache mpira kumalizika.

Mchezo huo uliofanyika Mbeya, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 
Credit to Udaku Specially
MaoniMaoni Yako