Ommy Dimpoz Ashushwa na Nandy


Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nandy ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Ninogeshe' amemshusha chini kwa nafasi moja katika mtandao wa Youtube msanii Ommy Dimpoz ambaye naye anafanya vyema na wimbo wake wa 'Yanje'.

Nandy sasa kwa upande wa Tanzania video yake imeshika nafasi ya kwanza katika mtandao huo wa YouTube na kumshusha Ommy Dimpoz ambaye alikuwa ana trend na kushika nafasi hiyo ya kwanza toka Mei 2, 2018 na sasa kushika nafasi ya pili chini ya Nandy.

Hata hivyo mapokeo ya video hiyo ya Nandy yamekuwa ni makubwa sana kwani video yake ndani ya siku sita toka ilipotoka Mei 3, 2018 imeshafikisha watazamaji zaidi ya Laki sita huku wengine wengi wakisema kuwa kupitia wimbo wake huo mpya na video yake hiyo imewafanya wasahau ujinga wake aliofanya wiki kadhaa zilizopita baada ya video yake akiwa faragha na Bill Nas kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.
Credit: Udaku
MaoniMaoni Yako