Nyota Jonas Mkude ateuliwa Balozi Kombe la Dunia

Dar es Salaam. Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amekuwa miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kuwa mabalozi wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia Star Times.
Mashindano hayo makubwa duniani yanatarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Russia.
Nyota Mkude ameungana na mchezaji wa Yanga, Ibrahim Ajib ambaye aliteuliwa pia kuwa miongoni mwa mabalozi kuelekea mashindano hayo.Star Times watakuwa wanaonesha mechi zote za michuano hiyo kupitia king'amuzi chao kuanzia Juni 2018. 
Hata hivyo baadhi ya nchi zilitishia kutaka kupinga mashindano hayo makubwa kutokana na kutokubaliana na sera za Rais wa nchi hiyo.
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako