Nimepata cheti cha kidato cha nne, sina mpango wa kugombea Simba – Hassan Dalali

Related imageAliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali amesema kuwa licha ya kuhitimu na kupata cheti cha kidato cha nne hana mpango wakuwania uongozi ndani ya timu hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali
Mwenyekiti huyo wazamani wa Simba, Dalali aliachia ngazi mwaka 2010 baada ya harakati za uchaguzi kumtaka mgombea nafasi hiyo ya juu kuwa angalau amefika kidato cha nne wakati yeye akiwa na elimu ya darasa la saba.
Ile kanuni ilipokuja mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Simba na wakati nafanya mabadiliko ya katiba nilikuwa Mwenyekiti wa mkutano ule nilikubali lifanyike hilo jambo ambapo kwa mtu mwingine ingekuwa ngumu sana.
Mimi nilijijua darasa langu la saba nikasema sawa hakuna tatizo tunakwenda na mabadiliko ya dunia sasa hivi.
Bila kukata tamaa akiwa na umri zaidi ya miaka 50, Dalali akaamua kurudi darasani kuitafuta elimu hiyo na kueleza kuwa licha ya kuhitimu na kupata cheti kinachomuwezesha kugombea uongozi wa juu ndani ya klabu ya Simba lakini hana mpango huo.
Ni watu wachache sana au watu wazima wachache ambao wanakubali kwenda darasani, kweli nimekwenda darasani nimesoma nimemaliza na vyeti nimepata nashukuru Mungu ijapokuwa watu wanasema sijapata ila nawaambia nimepata vyeti na nimefanya mitihani kupitia baraza la mitihani la taifa lakini sinamawazo ya kugombea ndani ya klabu ya Simba.
Dalali amesema pia licha ya Simba kuonyesha dalili za kutwaa ubingwa msimu huu bila kufungwa mchezo hata mmoja lakini bado haiwezi kufikia rekodi aliyoiweka akiwa kiongozi wa timu hiyo msimu wa mwak 2009/10.
Mwaka 2009/10 ndiyo tukachukua ubingwa bila ya kufungwa tulishinda mechi zote na kutoka sare mechi mbili hata Azam FC nayo ilichukua ubingwa bila ya kufungwa lakini ilitoka sare saba na kwa sasa hivi timu yangu ya Simba imeshatoka sare mechi nane hatujamaliza michezo minne hapo inamaana timu yoyote inayo taka kuvunja rekodi niliyoiweka chini ya uwongozi wangu lazima itoke sare moja tu kwahiyo rekodi yangu bado inakwenda tu ni kwamba haijavunjwa.
Hassan Dalali alichukua kijiti cha uongozi wa klabu ya Simba mwaka 2006 baada ya mgogoro wa kiutawala uliyoikumba timu hiyo kwa wakati huo.\

by richard@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako