Nilimpenda Diamond Sana ila Madharau yalizidi – Zari Afunguka


Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amesema alimpenda sana muimbaji huyo na kila mtu alifahamu hilo ila madharau yalizidi ndipo akaamua kuvunja mahusiano yao.

Zari katika mahojiano na Kiss FM nchini Kenya amesema kwa kuwaida mwanaume anaweza kuchepuka ila kwa Diamond dharau zilizidi na alihisi kama utu wake umeshushwa.

Ameendelea kwa kusema kuwa Diamond alikuwa akimkosea heshima katika mitandao ya kijamii na hakuwa na heshima kwa wanawake kitu kilichopelekea hata watoto wake kutukanwa na ukizingatia hawana baba hivyo hakuona sababu ya kuendelea na mahusiano hayo.

I loved him so much and everyone knows about that, you can go cheat there as a man but when it comes in with disrespect that is when it became too much. I felt that my integrity was so low.

Diamond misbehaving on social media, they will not have respect for women when they grow up. I asked myself, why do I have to settle low for this? My children were insulted on social media. Being the fact that they do not have a father, they will know that in future they need to respect women and that is why I left.

February 14 mwaka huu ndipo Zari alitangaza kuvunja rasmi mahusiano yake na Diamond Platnumz. Kwa sasa Zari upo nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ itakayofanyika weekend hii Uhuru Gardens.
Credit: Udaku