Neymar, Coutinho kuiongoza Brazil Kombe la DuniaLondon, England. Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia, Brazil imeonyesha dhamira ya kutwaa ubingwa mwaka huu.


Brazil imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mara tano na sasa inasaka kuweka rekodi katika fainali hizo.


Neymar, Philippe Coutinho na wachezaji wengine wa Brazil wanafanya mazoezi kwa kiwango cha juu kujiandaa na mashindano hayo. Juzi, nyota hao walionekana wakijifua kwa nguvu huku Neymar akiwa kinara wa mazoezi hayo.


Mshambuliaji huyo wa Paris Saint Germain (PSG), alionekana akiwa fiti wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja mpya wa Tottenham Hotspurs.


Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Roberto Firmino amejiunga na kambi ya Brazil baada ya kumaliza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya waliochapwa mabao 3-1 na Real Madrid.


Brazil inatarajiwa kuvaana na Croatia katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Anfield, Jumamosi mchana. Timu hiyo itafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Uswis Juni 17
MaoniMaoni Yako