Nay wa mitego atuhumiwa kwa ushirikina

Rapa B Gway mwenye 'hit song' ya 'Sijachukia' amefunguka na kudai msanii Nay wa Mitego alishawai kufanya jaribio la kuzuia mvua eneo la Tanganyika Pekazi Jijini Dar es Salaam katika tamasha lake la nguvu ya kitaa.

B Gway amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV  baada ya kutokuwepo na maelewano mazuri baina yao tangu alipotoka katika uongozi wa Freenation alipokuwa anasimamiwa kazi zake za muziki na Nay huku akidai kuna njama za kutaka kumpoteza katika tasnia hiyo.

"Unajua kibinaadamu ukifikilia halafu ukirudi kwenye dini yangu mimi ninaamini sana uwepo wa Mwenyezi Mungu, yaani naamini sana kwamba nitafika, kwa hiyo kama anaimani kwamba atatia tia ubani ili mimi mambo yangu yasiende basi ngoja tuone huo ubani utakavyokuwa. Ile nguvu ya kitaa kuna mambo mengi yameendelea kwasababu mvua ilikuwa inanyesha lakini kuna sehemu kulikuwa kweupe tu", amesema B Gway. 

MaoniMaoni Yako