Nampongeza Kaseja - Okwi

Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi, ametoa pongezi kwa golikipa wa timu ya Kagera Sugar, Juma Kaseja, kwa kufanikiwa kudaka mkwaju wake wa penati ambao ulipelekea timu ya Simba kupoteza mchezo wake wa kwanza katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara.
Okwi amesema  hayo jana Mei 19. 2018 akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika sherehe za kukabidhiwa kombe la ligi kuu na kuongeza kuwa anajisikia vibaya kutokana na kukosa mkwaju huo wa penati ambao umeharibu rekodi ya timu. Soma Zaidi
MaoniMaoni Yako