Mzee wa upako amtupia tena dongo kiba "Acheni uzinzi"

IKIWA ni siku chache baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ kumnanga Msanii Alikiba kuwa ana maringo tofauti na Diamond Platnumz ambaye alidai kuwa ni mtu mwenye upendo na watu wote, Kiba alimjibu mchungaji huyo kupitia Twitter.

  Mzee wa Upako  amesema msanii anatakiwa kuwa na adabu huku akisisitiza kwamba, ukimuuliza kiba swali huwa anajibu kwa madaha tofauti na Diamond huku akidai wasanii hao wawili ni kama watoto wake, hivyo hawezi kubishana nao mitandaoni.

“Wasanii wanatakiwa kuacha uzinzi, sio leo una mke huyu kesho unamke mwingine, utakufa. Walikuwepo wasanii wengi tu lakini jiulize nini kiliwashusha hadi wakapotea, tumeona wasanii wengi, usijione wewe ndiyo wewe,” alisema Mzee wa Upako.

Aidha, Mzee wa upako amesema wapo kuwa wasanii wengi wanaofanya vizuri nchini na siyo Kiba na Diamond pekee, wamewataja wengine kuwa ni Ben Pol, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’, Darasa na wengine 

MaoniMaoni Yako