Mpango wa Mo ibrahim kutua yanga wakamilika

Baada ya siku chache kudaiwa kuwa, kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ amesajiliwa Yanga imebainika kuwa dili hilo linatarajiwa kukamilishwa rasmi leo Jumatano, baada ya pande mbili kukutana na kuweza kumalizana.
Mo tayari ni mchezaji huru kwa sasa kutokana na mkataba wake kumalizika mwezi ujao na amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha Simba.
Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema anatara­jia kukutana na viongozi wa klabu hizo ili kuweza kujadiliana.
“Suala la Mo litafahamika rasmi kesho (leo) sababu mchezaji alikuwa kwenye mechi kule Songea na leo Jumanne (jana) ndiyo anarejea hapa Dar kwa mapumziko, hivyo kila kitu kuhusu yeye kitajulikana tu baada ya kuku­tana pande mbili sababu alipata ofa kadhaa.
“Sababu mkataba wake na Simba ndiyo huo unamalizika na ligi imekwisha, hivyo tutajua mustakabali wake kwa ujumla msimu ujao utakuwa ni kwa klabu ipi na tunacho­hitaji ni mchezaji kupata timu na kuweza kuendeleza kipaji chake,” alisema.
MaoniMaoni Yako