MOURINHO: Nitapitisha panga Man United

 KOCHA wa Man­chester United, Jose Mourinho amekiri kuwa kuna wachezaji ambao watalazimika kuondoka klabuni hapo kwa kutofikia levo za kuichezea timu hiyo inayomiliki Uwanja wa Old Trafford.

Inajulikana wazi kuwa Mourinho atafanya mab­adiliko kadhaa ka­tika kikosi chake ili kuweza kuwania ubingwa wa Pre­mier League am­bao msimu huu umeenda kwa wapinzani wao wa jiji moja, Manchester City.
 Ikumbukwe kuwa hivi kar­ibuni, amekuwa akiwakosoa An­thony Martial na Luke Shaw kwa kutocheza katika ubora anaou­taka huku uhusiano wake na Paul Pogba ukielezwa kuwa upo katika utata.

“Tunahitaji watu ambao wa­takuwa na mwendelezo mzuri uwanjani, tunataka watu am­bao wataondoa tofauti ili­yopo kati yetu na City.
“Najua kuna wachezaji watakaofikia kiwango ninachotaka na wengine hawatafika, ninalijua hilo.
“Unapofungwa na timu z i l i zopa nda daraja, kisha ukazifunga timu kubwa siyo dalili nzuri kwan­gu,” alise­ma Mour­inho.
Credit: Global Publishers

MaoniMaoni Yako