Mourinho aweweseka Chelsea kuwapiga FA


PENALTI ya Eden Hazard iliipa Chelsea ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA na kuifanya kutwaa taji hilo, lakini Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amekosoa mbinu za klabu yake hiyo ya zamani.
Mourinho anaona mbinu ya wapinzani wao hao ya "kucheza mipira mirefu" ni chanzo cha Chelsea kufanya mambo kuwa magumu kwa kikosi chake cha Manchester United  kwenye mechi hiyo ya FA.
Straika Romelu Lukaku - alianzia benchi kutokana na kutokea chumba cha majeruhi hivi karibuni katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Wembley juzi ambayo Hazard alizamisha mkwaju wa penalti kimyani dakika ya 22 kipindi cha kwanza.
Antonio Conte alimchezesha Hazard nyuma ya straika Olivier Giroud katika mfumo 3-5-1-1, huku safu ya kiungo cha ulinzi ikiwa chini ya N'Golo Kante.
"Nadhani timu yetu ilifanya kazi nzuri ya ulinzi," Mourinho aliuambia mkutano wa wanahabari. 
"Tulimiliki nafasi na kuzuia vizuri, walicheza mipira mirefu tu kwa kumpelekea Giroud, Hazard akifanikiwa kunasa mipira nyuma yake, na wakati unapocheza dhidi ya timu inayotabirika ni rahisi kuzoea hilo. 
"Sidhani kama tumeruhusu bao katika mechi hii, lakini bila shaka Hazard ni mchezaji mzuri sana na alitengeneza penalti."
 Credit: IPP Media
MaoniMaoni Yako