Mohamed Salah Ashinda Taji la Mchezaji bora tena toka kwa Waandishi wa Habari.

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na muungano wa waandishi.
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne alikuwa wa pili huku mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane akichukua nafasi ya tatu.
Salah, 25, amefunga magoli 31 katika mechi 34 za ligi ya Uingereza akiichezea Liverpoll msimu huu.
Nyota huyo wa Misri - ambaye ndio Mwafrika wa kwanza kushinda taji hilo 
Mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Fran Kirby alishinda taji la wanawake la mchezaji bora wa mwaka FWA.
Salah amefunga mabao 43 katika mashindano yote baada ya kusainiwa kwa dau la £34m kutoka Roma mwisho wa msimu.
Winga huyo wa zamani alifunga mabao mawili katika raundi ya kwanza ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya klabu yake ya zamani katika uwanja wa Anfield.
Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kinasafiri kuelekea Stadio Olimpico siku ya Jumatano kwa marudio ya raundi ya pili kikiongoza 5-2 dhidi ya Wataliano hao.
Salah na De Bruyne walipata 90% ya kura kutoka kwa wanachama wa muungano wa waandishi wa kandanda lakini Salah akashinda kutokana na mabao yake mawili aliyofunga dhidi ya Roma wiki iliopita.
Wachezaji wengine waliotarajiwa kupata kura kutoka kwa FWA ni: Sergio Aguero (Man City), Christian Eriksen (Tottenham), Roberto Firmino (Liverpool), Nick Pope (Burnley), David Silva (Manchester City), Raheem Sterling (Man City) na Jan Vertonghen (Tottenham).
Source:BBC
MaoniMaoni Yako