Thursday, May 3, 2018

MO Dewji amzuia Lechantre Simba

TagsSIMBA ni kama imebeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini mashabiki hawana imani kabisa kama kocha wao, Mfaransa Pierre Lechantre atabaki klabuni hapo.
Lenchantre anatajwa kuwania kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya Cameroon na anapewa nafasi kubwa kuebaba kibarua hicho, na hilo limeanza kuibua kelele za wana Simba.

Lakini, bilionea wa klabu hiyo ambayo amewekeza pesa ndefu kuhakikisha Simba inatamba Afrika, Mohamed Dewji (Mo) amesikia kelele hizo na fasta akafanya kitu amnacho kitaleta mzuka kwa mashabiki.

Kwa taarifa yako tu, Lechantre mwenyewe ameibuka na kuweka bayana kwamba, ataendelea kuwepo Msimbazi hata kama dili la Cameroon litatiki kwani, mpango mzima kuhusiana na hatima yake uko chini ya Mo.

Kocha huyo ambaye ana miezi mitatu tu tangu alipobeba mikoba ya kuinoa Simba kutoka kwa Mcameroon Joseph Omg, amesema ana mahusiano mazuri na mabosi wa Simba na kwamba, anapata kila aina ya sapoti anayotaka hivyo hawezi kuondoka kirahisi hivyo, ni lazima mabosi wa Cameroon wakubaliane kwanza na Simba.

"Nimekuwa na maelewao makubwa na viongozi wote wa Simba hasa Dewji na wamekuwa wakinisikiliza na kunipa ushirikiano kuliko sehemu nilizowahi kufanya kazi jambo ambalo nahisi nafanya kazi katika mazingira sahihi kabisa," alisema.
Mfaransa huyo akaongeza; "Mazingira ninayofanya kazi ni sahihi na naweza kuwepo hapa kwa muda mzaidi, ila kama Shirikisho la Cameroon litanipa kazi itabidi waongee na uongozi wa Simba kama watakubali kuniachia.

"Simba ndio mabosi wangu, pia nipo ndani ya mkataba wao, hivyo kama Cameroon itanihitaji watalazimika kuongea na viongozi wangu ili kupata muafaka," alisema.

Chanzo: Mwanaspoti