Mkutano Mkuu Yanga Wasogezwa Mbele


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuhusu mambo mbalim­bali ikiwemo mkutano mkuu uliokuwa ufanyike wikiendi hii.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, Ofisa Habari, Dismas Ten na Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga, Bakili Makele ndio waliohusika katika mkutano huo wa wanahabari uliofan­yika jana makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa.

Ten aelezea safari ya Alge­ria
“Kikosi cha wachezaji 20 ndicho kinaelekea Algeria kwa ajili ya mchezo dhidi ya USM Alger.
“Hatuna hofu na hali ya hewa ya Algeria, mchezo utaaanza saa 2:00 usiku kwao sawa na saa 4: 00 usiku kwa huku kwetu.”

Mkwasa kuhusu mkutano mkuu
“Kamati ya Utendaji ya Yanga ilikutana juzi, tumeamua ku­sogeza mbele mkutano mkuu uliokuwa ufanyike Mei 5, sasa utafanyika Juni 17, ajenda itakuwa juu ya kuziba nafasi ambazo zipo wazi.”

Kuhusu fedha za Caf
“Watu wanatakiwa watam­bue kuwa fedha zile hazi­tolewi ilimradi tu na badala yake zinatoka kwa utaratibu maalum baada ya kucheza mechi za makundi.”

Bakili Makele atoa neno
“Naomba wanachama wa Yanga kuziandaa kadi zao kwa kuzilipia ili ziweze kuwa hai kujiandaa na mkutano ili kupata haki yao ya msingi siku ya mkutano mkuu kwani tumepata maelekezo kutoka TFF na serikalini kuziba nafasi zilizo wazi.”
Credit to Global Publishers
MaoniMaoni Yako