Mkongwe Tigana atabili bingwa wa FA


Arusha. Nyota wa zamani Ally Yusuph “Tigana” ambaye aliwahi kukipiga Mtibwa Sugar, amesema kuwa anaipa Mtibwa nafasi ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na kuwa na wachezaji wenye uzoefu wa kucheza fainali mbalimbali.
Mwishoni mwa wiki kutakuwa na shughuli pevu zitakapokutana Singida United pamoja na Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali utakaopigwa Wwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani.
Aidha mkongwe mwingine, Itutu Kigi Makasi ambaye atamshuhudia kijana wake Kigi Makasi anayekipiga katika kikosi cha Singida United ameelezea kuwa mchezo huo utakuwa ni fahali kubwa kwake kuona vijana wanatimiza ndoto zao kama wazazi wao walivyofanya enzi zao.
Itutu aliyewahi kukipiga kikosi cha Simba, amesema kubwa ni kujiandaa kwenye mchezo ndio inaweza kuleta ushindi kwa kila timu ndio maana ni vigumu kwake kubashili mchezo kumalizika kwa ushindi wa aina gani wala kuwapa ushindi timu fulani.
“Kila timu iliyofika fainali ina maana wanauwezo mkubwa, atakayepita anatakiwa kujipanga kwa michezo ya kimataifa jambo ambalo linatuangusha watanzania, timu zetu kila mwaka kuwa wageni kwenye michezo ya nje kutokana na kuwa na vikosi dhaifu.”
MaoniMaoni Yako