Messi aitaja timu anayotaka kuchezea


Messi ambaye yupo nchini Argentina kwenye kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, ameyasema hayo kwenye mahojiano na mtandao mmoja ambapo pia ameweka wazi mpango wake ni kuchezea timu yake ya utotoni Newell's Old Boys.

"Siwezi kusaini Man City, nipo Barcelona na ndio timu pekee nitakayochezea barani Ulaya, siku zote huwa natamani kurudi kuchezea timu yangu ya Old Boys hapa nyumbani hata kwa miezi sita'', amesema Messi.

Messi mwenye miaka 30, ataiongoza Argentina kwenye fainali za mwaka huu akiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali katika Kombe la Dunia mwkaa 2014 nchini Argentina.

Hata hivyo Messi amesaini mkataba mpya ndani ya Barcelona ambao utamweka klabuni hapo hadi Novemba 2021. Mkataba huo una kipengele cha timu kulipa kiasi cha Euro 700 milioni, takribani shilingi Bilioni 2.
MaoniMaoni Yako