Monday, May 21, 2018

Meghan Apewa Pete Ya Princess Diana, Sherehe Yafanyika Usiku (Picha +video)

Tags

Kidole cha Meghan kikiwa na pete iliyokuwa inavaliwa na mkwewe, Princess Diana.
Moja ya mambo yaliyosisimua zaidi katika sherehe ya usiku wa ndoa ya Mwanamfalme Prince Harry na mkewe Meghan Markle, ni pale ambapo biharusi alipokabidhiwa pete aliyokuwa akivaa marehemu Princess Diana ambaye ni mama wa mumewe.  Ikumbukwe kuwa hata wakati Prince William (kaka yake Harry) anamwoa Cathy Midleton alipewa zawadi ya mkufu ambao pia ulikuwa ukitumiwa na Prince Dianna.
Fataki zikipigwa eneo la Frogmore House ambalo palifanyika sherehe za harusi ya Prince Harry na Meghan usiku wa kuamkia leo.

Harry akimfungulia mlango mkewe.
 Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu 200 waliokuwa katika ukumbi wa Frogmore na wengine 100,000 waliruhusiwa kufuatilia sherehe hiyo wakiwa nje ya ukumbi huo.

Prince Harry na Meghan wakiwa wameshikana mikono wakitoka kwenye jumba la mfalme linalojulikana kwa jina la Windsor Castle.

Gari aina ya Jaguar lenye namba za tarehe ya harusi E190518 ikimaanisha 19/5/2018 wakati ikiondoka katika kasri la mfalme kuelekea ukumbi wa Frogmore House.

ANGALIA VIDEO