Mbwana Samatta awaonya Serengeti Boys kufuatia ushindi wao wa kombe la CECAFA

Image result for MBWANA SAMATTAMshambuliaji wa Taifa Stars  na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amewaonya vijana wa timu ya taifa ya mpira wa miguu waliochini ya miaka 17, Serengeti Boys kwa kuwataka waache kubweteka kufuatia ushindi wa kombe la CECAFA mwaka 2018.
Mbwana Samatta
Samatta amesema anaamini kuwa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limewaandalia vijana hao mazingira mazuri hivyo ni wao tu kujitunza na kuongeza juhudi.
Tunamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa“ameandika Mbwana Samatta kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo kwa upande mwingine Samatta ametoa pongezi kwa Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA “Hongereni sana ‘Serengeti’ (u17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17“.

chanzo bongo5
by richard@spoti.co.tz