Sunday, May 13, 2018

Mbeya City yachekelea sare ya Prisons

Tags

Mbeya. Sare waliyopata timu ya Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons hii leo kwenye Uwanja wa Sokoine imeipa ahueni City kuwa kwenye msitari mwekundu wa kushuka daraja.
City imefanikiwa kufikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28, lakini rekodi yao siyo nzuri kwa mechi zote wanazokutana na wapinzani wao tangu 2014 baada ya kuambulia vichapo pamoja na sare.
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurwimo alisema sare hiyo imempa matumaini ya kubaki Ligi Kuu kwa msimu ujao.
Alisema “Hizi mechi mbili nilizosaliwa nazo hazinipi presha ingawa natakiwa kupambana zaidi ili kumaliza ligi nikiwa katika nafasi nzuri kimsimamo.”
Kwa upande wake Kocha wa Prisons, Mohammed Abdallah alisema lengo lake ilikuwa ni kuvuna pointi tatu mbele ya wapinzani wao ili kutimiza adhima yao ya kumaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu.
"Ingawa silaumu kupata sare hii lakini tulitaka tuendeleze rekodi yetu ya kuwatambia wapinzani wetu kwa kuwafunga kwa mzunguko mzims," alisema Abdallah.
Credit: Mwanaspoti