Tuesday, May 1, 2018

Mbappe amtaka Kante atue PSG

Tags


Paris, Ufaransa. Kylian Mbappe amesema Paris Saint-Germain wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante mwisho wa msimu huu.
Mshambuliaji Mbappe (19), alibainisha Mfaransa mwenzake anataka kucheza tena Ligue 1, akiwa na mabingwa hao.
Wakati alipoulizwa ni mchezaji gani mmoja angependa ajiunge katika klabu hiyo, aliimbia beIN Sports: "Kante, kwa mujibu wa mahitaji yetu na pia kiwango chake cha uchezaji.
"Nafikiri ni mchezaji anayeweza kuwa sahihi zaidi kwa timu yetu.
"Ni Mfaransa, mrudishe Mfaransa kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu cha mabingwa, itakuwa ni vizuri akija hapa.
"Nafikiri Wafaransa wote wanampenda N'Golo Kante, na itakuwa ni faraja kwake kuwa naye katika ligi yetu."
Kiungo Kante, 27, alijiunga na Chelsea akitokea Leicester mwezi Julai 2016, kwa gharama ya pauni 30milioni.
Chanzo: Mwanaspoti