Mashabiki wammwagia KIchuya minoti


Simba, Shiza Kichuya juzi Jumamosi aliwashangaza wengi baada ya kuamua kucheza na fedha ambazo alipewa na mashabiki wa timu hiyo.

Kichuya alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kili­kuwa ugenini kuvaana na Sin­gida United katika pambano la Ligi Kuu Bara lililopigwa katika Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Katika mchezo huo Kichuya mwenye mabao saba katika ligi hakufanikiwa kuanza ka­tika kikosi cha kwanza, hivyo kuanzia benchi akiwa na nyota wengine kadhaa.

Championi Jumatatu am­balo lilikuwepo uwanjani hapo lilimshuhudia Kichuya akim­wagiwa fedha na mashabiki mbalimbali wa timu hiyo kiasi kinachofikia shilingi laki mbili (200,000) ambao walimpa fedha hizo wakati nyota huyo akiwa benchini.

Kutokana na kutokuwa na sehemu ya kuzihifadhi fedha hizo, Kichuya alizikunja fedha hizo na kuzitia katika soksi zake na kuingia uwanjani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.

Simba walishinda mchezo huo kwa bao 1-0 na kuifanya kuen­deleza rekodi yao ya kutofungwa kwa msimu huu hadi sasa. Bao lao lilifungwa na Shomary Kapombe.

Musa Mateja, aliyekua Singida.
Credit: Global Publishers
MaoniMaoni Yako