MANARA: Siwezi kuishi bila mke wangu!!!


Ukitaka kumtesa msemaji wa Simba Haji Manara basi we mwambie aishi bila mke, amekiri mwenyewe kwamba hawezi kuishi bila mke.

Manara anasema tangu alivyooa ameshasahau kunyoosha nguo, kufua na mambo mengine kibao kwa sababu vitu vyote hivyo hufanywa na mama watoto wake.

Ukimuona Manara popote kama amependeza au ‘amepuyanga’ upande wa mitupio basi wa kusifiwa au kulaumiwa ni mke wake, jamaa anasema hadi nguo za kuvaa kwenye mitoko mbalimbali anapangiwa na baby wake.

“Wanawake wanafaida kubwa sana, kwa mfano ukizoea kuishi na mke, huwezi kuishi bila mke. Mimi siwezi kuishi bila mke, kwa sababu kuna baadhi ya mambo ya msingi kwa binadamu mimi siyamudu.”

“Siwezi kupiga pasi, kufua, sio kwamba sijui lakini nimeshasahu miaka nyingi sana. Sijawahi kufungua kabati langu la nguo kwa hiyo sijijui yani, hata nguo za kuvaa nachaguliwa na mke wangu, nikitaka kutoka ananiuliza mizunguko yangu halafu ananichagulia nguo za kuvaa.”

“Tangu nimeoa sijawahi kujichagulia nguo za kuvaa kwa hiyo kwangu kuishi bila mke ni shida. Namshukuru Mungu hata mtalaka wangu ambaye alikuwa mke wangu wa kwanza naye alikuwa hivyohivyo.”

“Namshukuru Mungu katika jambo ambalo sikukosea ni kuchagua mke, wa kwanza na wa pili pamoja na kwamba mke wa kwanza nimwacha lakini sikukosea, nimepata wake ambao dini zetu, kabila zetu, tamaduni zetu, wake wazuri ambao unaweza kutoka naye popote lakini na tabia zao nzuri.” 
Credit: Udaku
MaoniMaoni Yako