Manara Alimwa Barua ya ONYO kali na TFF, Kisa hiki hapa..

Dar es Salaam. Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania imempa onyo kali Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kutokana na kuingia uwanjani kabla na baada ya mechi yao dhidi ya Yanga.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Boniface Wambura alisema kwamba kamati hiyo ilipopitia jambo hilo na kuamua kutoa onyo kalikwa kiongozi huyo ambaye amekwa na makeke pindi timui yake inapokuwa inacheza.
Yanga ilikumbana na kipigo cha bao 1-0 kutoka Simba Jumapili ya wiki iliyopita na kufikisha idadi ya mapambano sita ya watani wa jadi bila kuonja ladha ya ushindi.

Source: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako