Mambo Muhimu Ya Kufahamu Kuelekea Kombe La Dunia..

umebakiza mwezi mmoja kuelekea kuanza kwa michuano ya kombe la dunia nchini Russia, tunaanza na wewe kuhesabu siku hizo huku tukikuletea mambo mbalimbali yahusuyo fainali hizo zinazotarajiwa kuteka hisia za wakazi wa sayari ya dunia.

Ni michuano inayokutanisha timu za taifa zilizofuzu kutoka nchi wanachama za Fifa. Michuano hiyo hufanyika kila baada ya miaka minne tangu ilipoanzishwa mwaka 1930. Haikufanyika mwaka 1942 na mwaka 1946 kutokana na zahama ya vita vya pili vya dunia.

Bingwa mtetezi wa sasa wa kombe la dunia ni Ujerumani ambaye alitwaa taji hilo mwaka 2014 nchini Brazil baada ya kuifunga Argentina kwenye mchezo wa fainali.

Timu shiriki zinapatikana kupitia mtindo wa kufuzu ambapo mchakato wake huchukua miaka mitatu na washindi hupata tiketi za kushiriki fainali hizo.

Nchi 32 hupata tiketi ikiwemo nchi mwenyeji ambayo hufuzu moja kwa moja, fainali hizo hufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Kombe la dunia limefanyika mara 20 ambapo mpaka sasa nchi nane zimetwaa taji hilo lenye hadhi duniani.

Brazil ndio nchi ambayo imetwaa taji hilo mara nyingi, limetwaa mara tano na ndio taifa pekee lililoshiriki kila fainali za kombe la dunia tangu mwaka 1930.

Washindi wengine wa kombe la dunia ni Italy na Ujerumani zilizotwaa mara nne kila mmoja, Argentina na bingwa wa kwanza wa kombe la dunia Uruguay zimetwaa marabmbili huku England, Ufansa na Hispania kila moja ikitwaa mara moja.

Kombe la dunia ndio kombe lenye thamani zaidi duniani na ndio shindano linalotazamwa zaidi na wapenda michezo wote duniani kote. Kombe la dunia la mwaka 2006 lililofanyika nchini Ujerumani ndiyo linaloongoza mpaka sasa kutazamwa na watu watazamaji zaidi huku zaidi ya watu milioni 715.1 wakitajwa kutazama mchezo wa fainali sawa na asilimia 19 ya wakazi wa dunia.
Chanzo: Shaffih

MaoniMaoni Yako