Monday, May 28, 2018

MAKUBWA: Kumbe Hamisa Mobeto anazima Nguo

Tags


UBUYU hauna saa hata ukiamka saa nane usiku unamung’unyika tu! Waswahili wanasema cha kuazima hakistiri makalio! Hayo ndiyo yamemkuta mwanamitindo maarufu aliye pia mzazi mwenza wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobeto ‘Tununu’ kutangaza nguo kuwa ameshona yeye, kumbe siyo kweli.

MAMBO YALIANZA HIVI;

Wiki iliyopita Wasafi TV ya Diamond iliandaa futari ambapo waliwaalika mastaa mbalimbali wa Bongo. Katika shughuli hiyo, Mobeto au first lady wa sasa akatangaza kwamba nguo aliyovaa siku hiyo aliitengeneza mwenyewe.

Hakuishia hapo, akaeleza kwamba hata nguo aliyovaa Sarah ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ yeye ndiye aliyehusika, kumbe sivyo.


MITANDAO YATIBUKA

Baada ya Mobeto kuposti picha yake na Sarah wakiwa wamevaa gauni zikionesha kuwa zimetengenezwa kwenye duka lake (Mobeto). Kumbe ndivyo sivyo kwani aliyezitengeneza ni mtu mwingine anayejiita Ab Desgners ambaye alimwandikia ujumbe mwanamitindo huyo kuwa awe mkweli.

MWENYE NGUO AFUNGUKA

Baada ya kuona mambo hayo yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii, Spoti TV, lilimtafuta mmiliki mwenye nguo hizo aitwaye Alliyah Abilliant ambapo alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo alifunguka hivi;

Spoti TV: Wasomaji wangetaka kufahamu hilo sakata la nguo likoje? Je, zimetoka kwako kweli?

Alliyah: Ni kweli nguo ni zangu kwani Mobeto alikuja kwangu na kunieleza kuwa anataka achukue nguo zangu avae alafu atasema zimetoka kwake ili anitangazie biashara.

Spoti TV: Sasa akutangazieje wakati amesema zimetoka kwake?

Alliyah: Ni kwamba akipata wateja aniletee, mimi nilikataa, nikasema kama anachukua nguo anitangazie kwa jina langu la sivyo nimuazime tu arudishe.


Spoti TV: Kwa hiyo ulipoona ameandika hivyo kwenye mitandao ya kijamii ulichukua hatua gani?

Alliyah: Nilimpigia simu, akaniambia yeye ana wafuasi wengi kwenye mitandao ndiyo walioandika vile hivyo hata ile ya Sarah, nikamuambia nimechukia kwani ameniharibia biashara yangu.

Spoti TV: Vipi ameshazirudisha hizo nguo?

Alliyah: Ndiyo, tayari amezirudisha.

Spoti TV: Asante.

Alliyah: Asante nawe pia.

HAMISA ANASEMAJE?

Baada ya Alliyah kufunguka, Spoti TV, kama ilivyo desturi yake lilimtafuta Mobeto ili afungukie madai hayo ambapo naye mambo yalikuwa hivi;

Spoti TV: Mobeto vipi kuhusu haya madai ya kusema nguo umeshona wewe kumbe siyo?

Mobeto: Jamani mimi nilishaeleza sana na hata nilipoweka kwenye mitandao niliandika kuwa nguo hizo zimebuniwa na yeye sasa mimi nashangaa watu wananichafua kwenye mitandao.

Spoti TV: Umefanya kitu gani sasa kutokana na hilo?

Mobeto: Nimewaacha tu maana huwezi kumuelewesha kila mmoja kwa sababu ukweli ninao mimi maana kuna watu wanatumia nguvu nyingi kuharibu jina langu.

Spoti TV: Asante sana Hamisa.

Hamisa: Poa.