Majonzi: Wachezaji wafariki dunia kwa ajali Mei Mosi

Mtwara. Msemaji wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Mtwara (Mtwarefa), Juma Mohamed amethibitisha kotokea kwa ajali iliyowahusisha wachezaji wa timu ya Mwena FC ya Ndanda wilayani Masasi.
Mohamed amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku wakati wakitokea kwenye maadhimisho ya Mei Mosi wilayani Newala.
Amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na kwamba taarifa za kina zitatolewa baadaye mchana.
Endelea kufuatilia tovuti yetu ya Mwanaspoti kupata habari zaidi.
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako