Majimaji yashuka, Ndanda yabaki ligi kuu


Dar es Salaam. Ama kweli Ng’ombe wa masikini hazai, ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Majimaji kushuka daraja rasmi na sasa wataungana na Njombe Mji kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wakati Ndanda ikisalia Ligi uu .
Majimaji imeshuka baada ya kumaliza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Simba wakati Ndanda imebaki baada ya kuichapa Stand United mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mshambuliaji chipukizi wa Majimaji, Marcel Kaheza ambaye tayari amemalizana na Simba kwa makubaliano ya mkataba wa awali, alipambana kuhakikisha timu yake ya Majimaji inabaki Ligi Kuu pale alipoipatia bao la kuongoza dakika ya 6, lakini kwa sababu bahati haikuwa yao, Simba ilisawazisha dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Haruna Niyonzima.
Kutokana na matokeo hayo, Ndanda imebaki Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 29 na kuicha Majimaji chini ikiwa na pointi 25.
Hata hivyo, katika mchezo mwingine uliokuwa na ushindani, Tanzania Prisons imeng'ang'ania kwenye nafasi ya nne baada ya kuifunga Singida United bao 1-0, mchezo uliopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Matokeo ya mechi nyingine Lipuli imeshindwa kutamba nyumbani kwao baada ya kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar, Mtibwa Sugar imetoka suruhu na Mbeya City, Njombe Mji imepoteza kwa Mwadui FC imechapwa mabao 2-0 na Mbao FC ikitoka sare ya 1-1 na Ruvu Shooting 'Wazee wa Kupapasa.Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako