Mabingwa Simba wakomaa sare ya 2-2 kwa Dodoma KombainiKlabu ya Simba leo Jumapili imebanwa mbavu kwa kutoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Dodoma Kombaini mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.


Bao la penati dakika za majeruhi la Kiungo Razak Khalfan ndilo lililoiokoa timu ya Dodoma kombaini ambayo ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1 awali ndipo walipopata penati hiyo na kuwapa bao la kusawazisha.


Mabao ya Simba leo yamefungwa na Shizza Kichuya kwa penati na Ally Shomary wakati mabao ya Dodoma yalifungwa na Anuary Jabir na Razack Khalfan kwa penati pia.


Baada ya mchezo huo Simba usiku leo watakuwa na sherehe maalum waliyoandaliwa na wabunge wapenzi wa timu yao ambao wapo jijini Dodoma wakati huu mikutano yake ikiendelea.
Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako