Liverpool yatinga fainali UEFA baada ya miaka 11


Liverpool imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tokea 2007 kwa jumla ya magoli 7-6 licha ya kupoteza mbele ya Roma kwa magoli 4-2.

Safari ya Liverpool ilianzia Ujerumani Agosti 15 ilipocheza na Hoffenheim na May 26 itachuana na Real Madrid mjini Kiev.

Licha ya kupoteza katika mchezo huo, ilikua shangwe kwa mashabiki wa Liverpool 5,000 waliosafiri kuhakikisha timu yao inapata nguvu ya ziada kutoka kwao kwenye dimba la Stadio Olimpico.

Klopp alikumbatia kila mchezaji wakati timu yake ikipiga picha ya pamoja baada ya mchezo.

Mashabiki wa Liverpool waliendelea kushangilia kwa nguvu hata baada ya mchezo kwisha huku wakisalia kwenye jukwaa lao.

Wakiwa na faida ya magoli 5-2 katika mzunguko wa kwanza nyumbani Anfield, Liverpool ilianza kujipatia goli lake kupitia Sadio Mane baada ya pasi safi ya Roberto Firmino.Mashabiki wa Liverpool waliendelea kushangilia kwa nguvu hata baada ya mchezo kwisha huku wakisalia kwenye jukwaa lao.

Wakiwa na faida ya magoli 5-2 katika mzunguko wa kwanza nyumbani Anfield, Liverpool ilianza kujipatia goli lake kupitia Sadio Mane baada ya pasi safi ya Roberto Firmino.

posted by Lebab
Chanzo: BBC

MaoniMaoni Yako