Liverpool, Arsenal zawashika pabaya Chelsea, Spurs


London, England. Chelsea na Tottenham Spurs wanaweza kukosa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao hata kama watamaliza katika nafasi ya nne.
Mbio za kuwania nafasi nne za juu za Ligi Kuu England zimepamba moto katika wiki za karibuni.
Liverpool akili yao ipo katika Ligi ya Mabingwa jambo lililowafanya wapoteze pointi ugenini dhidi ya West Brom na nyumbani dhidi ya Stoke.
Huku Manchester City na Manchester United wamejihakikishia nafasi mbili za kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, huku Arsenal ikiwa imejiondoa katika mbio hizo hivyo kuacha vita wa timu tatu kuwania nafasi mbili zilizobaki.
Kikosi cha Jurgen Klopp kipo mbele katika mbio hizo, lakini Chelsea na Tottenham wakikabana koo.
Lakini hata kama mmoja wapo kati ya Chelsea au Spurs akimaliza nafasi ya nne anaweza kukosa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao… hivi ndivyo itakavyokuwa.
Endapo Chelsea na Tottenham zitamaliza juu ya  Liverpool, na miamba hiyo ya Anfield ikiondolewa katika nne bora, lakini wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa na Arsenal akatwaa ubingwa wa Europa Ligi.
Katika mazingira hayo, England itakuwa na timu sita zilizofuzu kucheza mashindano hayo makubwa Ulaya.
Hata hivyo, sheria ya Uefa inaruhusu timu tano tu kutoka katika nchi moja kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa.
Hiyo inamaana yoyote anayemaliza  katika nne bora kati ya Chelsea au Tottenham hatoweza kufuzu kwa mashindano hayo makubwa ya klabu Ulaya.
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako