Lampard aishusha Real Madrid kwa Liverpool

London, England. Licha ya kupenya katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Frank Lampard amesema Real Madrid haina ubavu wa kuifunga Liverpool.
Lampard alisema Real Madrid haina kiwango cha kutisha kulinganisha na Liverpool na endapo timu hizo zitacheza fainali kocha Jurgen Klopp ataondoka uwanjani na kicheko.
Kauli ya nguli huyo wa zamani wa Chelsea na England, imekuja muda mfupi baada ya Real Madrid  kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Bayern Munich ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Real Madrid inayonolewa na kocha Mfaransa, Zinedine Zidane, ilisonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Lampard, Rio Ferdinand na Steven Gerrard walisema Bayern Munich ilistahili kucheza fainali baada ya kuangalia kiwango cha Real Madrid katika mchezo wa juzi usiku.
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako