Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa – Alikiba


Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amesema licha ya umaarufu mkubwa alionao ataendelea kuishi maisha ya kawaida ya kutojionyesha (show off).

Muimbaji huyo katika mahojiano na Dj Show ya Radio One amesema kuwa maisha anayoishi ndio anaona yanafaa zaidi machoni kwa mashabiki wake ambao walimpokea kipindi hana kitu.

“Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa. Mimi sijachagua in nature nipo hivyo, Watanzania walinipokea katika hali ambayo kiukweli haisemeki sasa hii leo nije nibadilike, so nisingependa kumshawishi shabiki yangu kwa namna yoyote ile kuwa nimebadilika kwa sasa hivi,” amesema.

“Kwa hiyo ule wivu wa kumfanya mtu anze kunichukia kwamba Ali amekuwa hivi na hivi, hapana!. Mimi ni staa, mimi ni supa staa nitafanya, ninaishi maisha ambayo nimechagua lakini bado nitaendea ku-humble kwa watu,” ameongeza.

Alikiba kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mvumo wa Radi.
Credit: Bongo 5
MaoniMaoni Yako