Kilichomtokea Chemical Baada ya Kuvuta Sigara Kwa Mara ya Kwanza

Binti ambaye ni mkali wa 'Rap' nchini Chemical, amekiri kuwahi kujaribu kuvuta Sigara lakini aliacha baada ya kukohoa sana na hajawahi tena kurudia kitendo hicho.


Akiongea leo KIKAANGONI kupitia Ukurasa wa Facebook wa East Africa Television, mkali huyo amesema kwenye maisha watu hupitia vitu mbalimbali lakini kwake aliwahi kujaribu kuvuta Sigara lakini hakuendelea.

''Sigara nilishajaribu lakini nilikohoa sana sikuweza kuendelea, mimi nina tatizo sana la moshi kuingia mwilini kwangu kwahiyo vitu kama hivyo siviwezi na situmii tangu siku niliyojaribu'', amesema.

''Aidha Chemical amefunguka pia kutotumia kilevi cha aina yoyote kwenye maisha yake. ''Situmii kilevi zaidi natumia tu maji mengi lakini vilevi si vitu vya aina yangu'', ameongeza.

Mbali na hayo pia leo ameachia Video yake mpya inayoitwa 'Africa Heritage' ambapo imetambulishwa rasmi kwa mara ya kwanza KIKAANGONI na kueleza kuwa ni moja ya kazi zake anazoamini siku moja zitamfanya akumbukwe na jamii.