Kichuya apewa mchongo


KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amekifuatilia kiwango cha Shiza Kichuya tangu ajiunge Simba, kisha akamshauri winga huyo kuwa pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo katu asisahau kuweka nidhamu mbele ili asonge mbele zaidi.
Katwila alisema Kichuya amekuwa katika kiwango cha juu na nyota yake inaonekana kung’ara maradufu kwa kila mdau wa soka, hivyo awe mwangalifu asipotezwe na sifa anazopewa kila kona.
“Asilimia kubwa ya nyota wa Tanzania wanapotezwa na sifa, ila kwa mtu makini akiziepuka na kuongeza bidii lazima afike mbali na ndivyo namtaka Kichuya afuate nyayo hizo, ili awafikie kina Simon Msuva anayecheza Morocco na Mbwana Samatta aliyeko Genk ya Ubelgiji.” Katwila alimtolea mfano straika kutoka Uganda wa Simba, Emmanuel Okwi kwamba tangu aanze kucheza ligi ya Tanzania, jina lake liko juu na halewi sifa.
Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako