Kaheza aahidi makubwa Simba

BAADA ya kusaini mkataba mpya wa kurejea Simba, mshambuliaji, Marcel Kaheza, ameahidi kuisaidia timu yake kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa itakayoshiriki.
Kabla ya kwenda Majimaji, Kaheza alikuwa ni mchezaji wa timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 maarufu Simba B.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kaheza alisema sasa ameiva na yuko tayari kupambana kuisadia Simba iweze kufanya vema kutokana na kupata uzoefu.
Kaheza alisema ameshakuwa mzoefu na anaifahamu vema Ligi Kuu Bara pamoja na changamoto zake tofauti na awali alivyokuwa Simba.
"Napenda kuwaahidi kuwa ninakuja Simba kivingine, nimekua na ninaweza kupambana, kipindi kile ilikuwa ni sababu ya umri na wachezaji waliokuwapo wakati ule, nawaahidi nitaisaidia kupata mafanikio zaidi," alisema mshambuliaji huyo.
Aliongeza kuwa anaweza kuitumikia klabu hiyo katika mazingira yoyote kwa sababu anaamini changamoto katika soka la Afrika ni jambo la kawaida.
Mbali na Kaheza, wachezaji wengine wapya wanaotajwa kusajiliwa na mabingwa hao ni pamoja na Adam Salamba kutoka Lipuli ya Iringa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya wakati mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wao wamemnasa, Donald Ngoma kutoka Yanga.
MaoniMaoni Yako