Kagera yasema itawafunga simbaKikosi cha Kagera Sugar kitakuwa mgeni wa mchezo wa ligi dhidi ya Simba Mei 20 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kagera inajiandaa kucheza na Simba baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono katika mechi ya mwisho dhidi ya Njombe Mji kwa kuifunga mabao 3-1.

Ushindi huo umekuwa ni salaam ya kuja kutibua rekodi ya Simba ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye ligi msimu huu.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Ally Jangalu, amesema kuwa ushindi dhidi ya Njombe unawapa nguvu ya kuzidi kufanya vizuri katika michezo ijayo ikiwemo Simba.

Ikumbukwe katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa January 22 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Kagera, Simba waliibuka na ushidi wa mabao 2-0.

Janagalu amesema hivi sasa wanajipanga kuja kulipiza kisasi ili kuwaharibia Simba ambao hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako