Jibu la Lulu Diva kuhusu kumzalia Rich Mavoko, hapo hapo atangaza ndoa

Muimbaji Lulu Diva amefunguka ukweli wa taarifa za kumzalia mtoto Rich Mavoko mwaka huu.

Muimbaji huyo amesema taarifa hizo si za kweli ila anahitaji atapokuwa tayari kufanya hivyo awe na muda wa kutosha tofauti na sasa ambapo muziki umemtinga.

“Ni ungo bwana!, nahitaji mtoto wangu ambaye nitazaa apate time yangu na pia baba mtoto awe tayari,” Lulu Diva ameiambia Uhondo, E FM.

Alipoulizwa kuhusu kuolewa, alijibu; ‘Soon naolewa lakini bado after miaka mitatu’.

Katika hatua nyingine amekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko, huku Mavoko naye akieleza kuwa na mahusiano yake ambayo yamempatia watoto wawili.

Lulu Diva na Rich Mavoko kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Ona. 
Credit: udakuspecially
MaoniMaoni Yako