Sunday, May 27, 2018

Je! Wajua? Hii ndiyo tofauti kati ya Mwanaume na Mwanamke ukiachana na Jinsia.

Tags

Ukifuatilia matukio mengi maovu ya kiubinadamu utagundua kuna tofauti kubwa ya utekelezwaji kati ya yale yaliyotendwa na mwanamke na yaliyotekelezwa na mwanaume.

Sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho mbaya ni unafiki na sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho ngumu ni ujasiri, pili sifa nyingne iliyopo kwenye kivuli cha unafiki ni uoga. 

Ukichunguza utagundua ya kua mtu mwenye roho mbaya ni mwoga na ndo maana analazimika kua mnafiki kuficha maovu yake na sifa ya pili ya mwenye roho ngumu ni kutojali/ogopa.

Tuangalie mfano mwanamke akitaka kufanya mauaji labda kwenye familia yake, atafanya hivyo lakini atafanya kwa njia ambayo hatataka kujulikana, mfano anataka kuua familia basi atatia sumu kwenye chakula halafu atajitia anakula na nyie(unafiki) mkizidiwa anajua kabisa haponi mtu anapiga mayowe kuita majirani na kwenye kesi akihojiwa tu anaanza kulia(unafiki grade A)

Je ushawahi sikia mwanaume anatia sumu kwenye chakula? Mwanaume anacharanga panga wote mkiwa mnamwangalia halafu anatia kwenye kiroba anazika(roho ngumu). 

Ukamletea mwanamke mtoto wa kambo hatakataa kuishi nae ila anachomfanya pindi haupo, ndo yale unaskia kalazmishwa kula kinyesi chake au mkojo, kachomewa madaftari, kanyimwa chakula, kachomwa na pasi, kafungiwa ndani n.k.

Halafu anatishiwa ole wako mtu ajue, baba akija anacheka na wewe(unafiki), ushasikia mwanaume anamnyima mtoto wa kambo chakula au kumlisha kinyesi? Labda ndio je mara ngapi? Mwanaume atakuambia wazi waz sitaki mtoto wa kambo(roho ngumu) nayo na mara chache.

Wanaume kuongoza kua wengi gerezani si kwamb a wao ni waovu sana kuzidi wanawake, kuna wanawake wengi sana wanapaswa kua kule ila unafiki ndo unawabakiza majumbani.

Source: Jamii Forum