Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Huyu Ronaldo ana kazi moja tu… na hakuna namna inabidi tumpende tu!Na Eston
        Hakuna unachopewa wala utachopewa kila kitu kinatafutwa.‘’Kutoka sifuri mpaka kuwa shujaa’’(from zero to hero) kilikuwa kibao moja matata kutoka kwa mwanadada Sarah Connor mapema mwanzoni mwa mwaka 2005 na ilikuwa moja ya kazi nzuri zilizowahi fanywa na Rob Tyger. Achana na maneno mengi yaliyokuwa ndani ya wimbo huo, jina la wimbo huo lilitosha kuupa uzito wimbo huo masikioni mwa watu.

        Ni nini kwani watu wanachokiheshimu zaidi kutoka kwa mtu asiefaa kitu leo? ,ni ushindi wa mafanikio yake ya kesho!!.Tangu mwanzo wa ulimwengu na kuendelea imekuwa hivo na itaendelea kuwa hivo imekuwa njia pekee ya watu walionekana sio kitu leo kujenga heshima yao kesho. Huna sababu ya kumchukia mtu wa ina hii mimi binafsi ninawaheshimu sana watu wa aina hio bila kujali maisha yao kiujumla ili mradi tu jana walikuwa sifuri mfukoni na leo ni mashujaa.
      Cristiano Ronaldo Do Santos Aveiro ni mmoja ya watu hao ni aina ya watu ninao waheshimu sana ni aina ya watu wale aliowaimba yule mwanadada wa kijerumani(Sarah Connor). Ronaldo aliezaliwa na mama mpishi Maria Dolores na baba yake aliekuwa mtunzaa bustani ya manispaa Jose Dinis Aveiro na mraibu wa pombe , maisha yake yalionekana kutofaa kitu wakati wa udogo wake yalikuwa sifuri kweli kweli. Ronaldo aliekulia katika familia ya kikatoliki alifikia hatua ya kuchangia chumba kimoja na dada zake na kaka zake .

      Akiwa katika ukuaji wake wazo pekee la ukombozi wake na familia yake lilikuwa soka. Kwa kutambua hilo akiwa na miaka 12 alienda kufanya majaribio katika moja ya klabu bora muda wote nchini ureno Sporting Cp. Majaribio ya siku 3 na hatimae waliliridhia uwezo wake na kumsajili na mapema akajiunga na timu ndogo ya vijana ,Ronaldo alieamini sana uwezo wake katika mpira wa miguu alifikia makubaliano na mama yake ya kuacha shule na kujikita zaidi katika masuala ya soka zaidi.
     Kwa kweli huyu Ronaldo  tunaeomwongelea leo ni habari nyingine kabisa kufikia hatua ya kupenya tiimu ya wakubwa ya  Sporting na kufanya vizuri na kutumia vema kila nafasi iliotokea mbelea yake hasa mechi ya kirafiki dhidi ya klabu yake ya baadae Manchester united ilibadili maisha yake kiujumla ulikuwa mwanzo wa kumtoa kwenye sifuri kuelekea kuwa shujaa ni kama timu nzima ya Manchester iliridhia usajili wake baada ya mechi yao ya kirafiki na Sporting kina Ferdinand walikuwa wana kazi moja tu kumuuliza Fergueson alichoona toka kwa Ronaldo Hawakuamini alikuwa ni kijana wa miaka 18 tu aliekuwa akiwanyanyasa vile.

      Kuingia united iliokuwa imara wakati huo na kupenya moja kwa moja hadi kikosi cha kwanza kilichozungukwa na wakongwe kibao kama kina Louis Saha,Ruud Van Nistelroy,Ryan Giggs na Diego Forlan halikuwa suala gumu kwa Ronaldo wakati huo. Kuwa mchezaji bora wa dunia akiwa na miaka 22 tu bado halikuwa suala gumu kwa Ronaldo na hatimae kutua kwenye viunga vya Bernabeu. Ronaldo huyu wa Madrid ameshafanya kila kitu na bado ana kiu sana akiwa na umri wa miaka 33 bado tamaa yake ni ile ile haridhiki hata kidogo. Unamuongelea mfungaji bora wa muda wote ndani ya klabu ya Madrid , unamuongelea mchezaji alieipa Madrid makombe 14 ndani ya miaka 9 aliyokaa klabuni hapo Ronaldo ameionjesha Madrid kila aina ya kombe iwe ni la liga(mara 2),copa del rey(mara 2),ligi ya mabingwa barani ulaya(mara 3),kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu(mara 3) ,Uefa super cup(mara 2).

   Unamuongelea mchezaji pekee duniani kufunga magoli zaidi ya 60 kwa kila mwaka ndani ya miaka 4 mfululizo(2011-2014). Na mchezaji pekee kufunga magoli 50 au zaidi ndani ya miaka 7 mfululizo , kuwa mchezaji wa kwanza kuwa mfungaji bora wa ulaya katika ligi mbili tofauti, mchezaji wa 1 kufikisha magoli 100 katika ligi ya mabingwa ulaya ,mchezaji wa 1 na pekee kufunga mechi zote katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ulaya, mchezaji pekee kufunga katika mashindano ya ulaya kwa ngazi za taifa 4 tofauti mfulilizo,hat-tricks nyingi ligi ya mabingwa ulaya, pasi za mabao nyingi zaidi ligi ya mabingwa ulaya, hat-tricks nyingi la liga, mchezaji wa kwanza kufikisha goli 300 kwa haraka zaidi katika historia ya la liga, pasi nyingi za mabao la liga… yaani hatutamaliza matukio yote ya  kijana huyu wa Madeira.

     Amefanya mengi sana makubwa! Yanayotosha yeye kuitwa  shujaa tena shujaa alieonekana kutofaa kitu udogoni mwake.Jambo la kufurahisha zaidi hata leo akiwa na miaka 33 bado anafanya makubwa kuna kitu kimoja Ronaldo anataka fanya msimu huu itakuwa ni adhabu  kwa  kizazi kinachofata  mwanzoni ilikuwa vigumu sana kuamini kuwa kuna timu ingeweza kutetea ubingwa wake wa ulaya sasa hilo sio jambo gumu tena Ronaldo anataka afanye hivyo kwa mara ya 3!!! Kama Ronaldo ataweza kufanya hivi ni nani  anaeweza kusimama na kukataa Madrid ndio timu bora karibu Muongo mzima? Ni nani anaeweza kuendelea kutafuta dosari yoyote ndani ya mchezaji huyu? Na bado akasimama na kusema yeye ni mpenzi wa kweli wa soka na sio mpenzi wa timu fulani au mchezaji fulani na bado watu wakamuelewa? Hakuna na hakuna!! Sahau ushabiki wote uliopo kati ya Cristian na Lionel na uruhusu moyo wako uongee , sahau ubishoo wake wote Ronaldo na maisha yake ya matanuzi sana yanayoweza kukukera mtazame Ronaldo wa ndani ya uwanja tu.

      Iliwahi kufikia hatua madridista wote pale Bernabeu walinyanyuka walau kwa dakika moja na wakampigia makofi Ronaldinho Gaucho mioyo yao ilizishinda akili zao wakasahau uhasimu mkubwa walio nao dhidi ya Barcelona walifanya tena miaka ya karibuni dhidi ya Andres Lujani Iniesta na bado sijachoka kusubiri naamini kuna siku watafanya hivyo tena mbele ya baba Thiago(Messi). Ndivyo soka lilivyo wakati mwingine inabidi ufurahie kilicho bora bila kujali nani anafanya hivo, Cristian nae msimu huu alipata heshima hio mbele ya wana Turin bao lake la tikitaka liliwakosha sana wakasahau walikuwa nyuma kwa goli 2 wakasimama wakampa heshima yake.

     Kama ubingwa utaanguka tena kwa vijana wa zizou ruhusu moyo wako ufurahie hilo hata kwa muda mfupi, sio rahisi mimi na wewe kuona timu nyingine itakayorudia kufanya hivo katika kipindi cha maisha yetu. Kutoka sifuri mpaka kuwa shujaa una kila sababu ya kuvutiwa na upambanaji wake Ronaldo ni kitia moyo na mfano bora kwa watoto wote wa ghetto wanapitia msoto mkali leo. Ni kama anawaambia kesho yao inaweza kuwa bora sana, Ronaldo ndio maana yote ya kibao cha Sarah Connor”from zero to hero”.

      
       


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post