Huu ndiyo Muonekano Mpya wa Mtoto wa Hamisa Mobeto na Diamond Platnumz

Dar es Salaam. Mwonekano mpya wa mtoto wa mwanamuziki maarufu Nasib Abdul (Diamond) na mzazi mwenzake Hamisa Mobeto umepamba mitandao ya kijamii baada ya kuamua kumuonyesha hadharani.
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Daylan ameonyeshwa kwenye mitandao hiyo na mama yake siku mbili zilizopita ambapo mashabiki wa wazazi wake walishangaa kumuona amekua haraka.
Mara ya mwisho kupostiwa mtoto huyo kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa Februari 22 jambo ambalo ni tofauti na mastaa wengine wanavyofanya kuposti watoto wao mara kwa mara.
Watu wengine walienda mbali zaidi kuhusu mwonekano wa mtoto huyo wakishindwa kutambua kwamba amefanana na mzazi wa kike au wa kiume.
Hata hivyo wengine walisema kwamba mtoto huyo kafanana na baba yake kwa sura lakini weupe kachukua kwa mama yake mzazi.
 “Hey baba ushakua sasa, Hamisa Mobeto anataka zawadi,’’aliposti Mobeto kwenye Intagram yake.

Source:Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako