Hatimaye "Mo" Akubali Kuimiliki Simba! Simba sasa mikononi mwa "MO"

MFANYABIASHARA na Mwanachama wa Simba, Mohammed Dewji 'Mo' amekubali kuimiliki klabu hiyo kwa asilimia 49 ya hisa.
Awali, ilitambulika kuwa Mo anaitaka Simba na alikuwa tayari kunua hisa 51 lakini baadaye serikali ilitoa maelekezo katika mpango huo na ikipendekeza kuwa umiliki wa hisa kwa mtu mmoja ni asilimia 49 tu.
Lakini, msemaji wa timu hiyo, Haji Manara ameweka wazi kuwa, Mo yuko tayari kuichukua Simba kwa asilimia  hizo 49: "Mo hajakataa kuimiliki Simba kwa asilimia 49."
Awali, Mo alipita kwenye kinyang'anyiro hicho cha akitaka asilimia 51 ya hisa na kwa ofa ya Sh 20 bil. Pia, aliahidi kuitoa timu kwenye bajeti ya Bilioni 1.2 kwa mwaka hadi Bilioni 5.5
Source: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako